Otile Brown wa Kenya ashangilia ngoma Dudusuma kufikisha Views Million 10 YouTube ndani ya siku 90

8 0

Dudusuma ni kati ya kazi ambazo zimemueka juu msanii mkali wa Kenya Otile Brown. Kazi hii ambayo alimshirikisha staa wa mzaliwa wa Rwanda na mwenye makazi yake nchini Marekani maarufu kama Meddy haijamtangaza Otile kimataifa pekee lakini pia imemufungulia mlango wa neema.

Hii ni baada ya miezi mitatu toka ngoma hii kupandishwa kwenye channel yake ya YouTube, kazi hii imetazamwa zaidi ya milioni kumi na mashabiki. Otile Brown ametumia mtandao wake wa instagram kuelezea furaha yake kwa kifikia kiwango hiki. Hatua ambayo inazidi kuwapa mhaho na kuwanyima usingizi wapinzani wake kimuziki.

Ikumbukwe kwamba mwanzoni mwa mwaka huu, kampuni ya YouTube ilitoa twakwimu zake za wasanii wenye views nyingi zaidi nchini Kenya. Na mkali huyu ambaye kwa hivi sasa anatamba na ngoma Ndagukunda aliyomshirikisha rapa mkongwe Africa mzaliwa wa Kenya maarufu kama CMB Prezzo, amezidi kuonyesha ishara zakutorudi nyuma huku mashabiki wake wakivamia akaunti yake ya instagram kwa kwikwi za pongezi baada ya kutupia post iliyootangaza hatua hii yake ya mafanikio miezi mitatu baada ya kuachia kibao hiki.

Imeandikwa na muandishi @changez_ndzai – Kenya

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *