Pierre Alivyojiachia na Warembo 3 Usiku

5 0Pierre Alivyojiachia na Warembo 3 Usiku

 

STAA aliyejizolea umaarufu kwa staili ya kupiga mitungi, Pierre Konki Liquid Ijumaa iliyopita, aliwashangaza watu kutokana na hekaheka zake alipokuwa akihangaika na warembo tofauti.

 

Pierre alinaswa na paparazi wetu kwenye shoo ya staa wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar. Kwenye shoo hiyo, Lady Jaydee alikuwa akisherehekea kutimiza miaka 20 ya muziki wake.

 

Ndani ya ukumbi huo, Pierre alinaswa na kamera ya paparazi wetu, akionekana kuwakumbatia warembo tofauti na kupeana nao pozi za kimahaba.

 

Paparazi wetu aliyekuwa akisaka matukio ukumbini humo, awali alimnasa akiwa amemkamatia kiuno mrembo fulani ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, wakipeana mapozi na tabasamu za hapa na pale.

 

Baada ya muda, alionekana akiwa na mrembo mwingine wakiwa wamekaa vitini, huku wakiangaliana kimahaba, wakichekeana huku wakipiga kilaji.

Pierre ambaye alijipatia ustaa kutokana na staili yake ya kupiga ‘maji’ huku akilalamika, katika shoo hiyo alionekana kupiga maji ile kama ilivyo kawaida yake. Akiendelea kuonesha ukali wake kwa watoto wazuri baada ya kumalizika shoo hiyo, Pierre alionekana kakumbatia kifaa kimoja na kuonekana wakiondoka kusikojulikana.

 

Wakati Pierre akiondoka na kifaa hicho, warembo wengine walionekana kumuita staa huyo ambaye hakuwa na taimu nao, akasepa zake.

 

Baada ya kushindwa kutoa ushirikiano kutokana na ‘ubize’ aliokuwa nao, mwanahabari wetu alizungumza na shabiki mmoja wa Pierre, ambaye alisema huenda warembo hao wote wanapenda tu kampani yake na si vinginevyo.

 

“Wewe humjui Pierre, anapendwa sana na warembo na si kuwa nao kimapenzi, zaidi huwa wanavutiwa na kampani yake tu,” alisema jamaa huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Kite.

STORI RICHARD BUKOS, RisasiToa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *