Pogba Ashtua Kukutwa na Corona

KIUNGO Paul Pogba amewashtua wadau wengi wa soka baada ya kubainika kuwa na Virusi vya Corona huku Ligi Kuu ya England ikitarajiwa kuanza ndani ya wiki mbili zijazo.

 

Kiungo huyo wa kati aliondolewa katika kikosi cha Ufaransa baada ya vipimo kubainisha kuwa ana corona, yeye Pamoja na Tanguy Ndombele wa Tottenham, muda mfupi baada ya kutua kambini.

 

Pogba sasa atalazimika kukosekana kwenye tukio la kuzaliwa mtoto wake wa pili Sasa Pogba, 27, atalazimika kujitenga kwa angalau siku 10 na atakosekana wakati Manchester United ikianza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya Jumatano ijayo.

 

Aaron Wan-Bissaka naye atakosekana siku za mwanzo za mazoezi kwa kuwa naye atalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kurejea akitokea mapumzikoni Dubai.Habari za corona ya Pogba zimekuja baada ya mlipuko wa virusi hivyo katika kikosi cha Chelsea ambako wachezaji sita walirejea wakiwa na corona.

 

Mason Mount, Tammy Abraham, Christian Pulisic na Fikayo Tomori wote inaelezwa wapo karantini. Premier inaanza SeptembaToa comment