Polepole Aeleza Maendeleo ya Belle 9, Lulu Diva

KATIBU  wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole,  leo Septemba 8, 2020,  amesema wasanii Bonge la Nyau, Lulu Diva na Belle 9 wameshatoka hospitali na wanaendelea vizuri.

 

Wasanii hao walipata ajali ya gari maeneo ya Chalinze alfajiri ya kuamkia siku ya Septemba 7, 2020,  wakati wanarejea Dar es Salaam baada ya kutoka kwenye kampeni za CCM, Kilolo mkoani Iringa.

 

Akitoa taarifa hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter, Humphrey Polepole ameandika kuwa,

“Napenda kuwajulisha kuwa vijana wetu Belle9, Bonge la Nyau wameshatoka hospitali na binti yetu Lulu Diva wote wanaendelea vizuri, Lulu Diva tunaomba Mungu atatoka hospitali leo, ahsante wote kwa support, ahsante zaidi Ummy Mwalimu, Muhimbili Taifa na Rais Magufuli, Mungu awabariki”Toa comment