Precision Yasitisha Safari Zake Kenya

SHIRIKA  la Ndege la Precision Air limetangaza kusitisha kurejeshwa kwa safari zake za Nairobi nchini Kenya kutokana na uhitaji mdogo. Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema watatangaza ratiba mpya hivi karibuni.

 

Uamuzi huo unakuja siku chache baada ya gazeti la Business Daily kumnukuu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Safari za Ndege (KCAA), Gilbert Kibe, akisema kampuni ya Precision Air ina haki za usafiri ambazo hazitaathirika licha ya sintofahamu iliyopo kati ya Tanzania na Kenya.

 

Mamlaka ya Usalama wa Anga (TCAA) imezuia mashirika manne ya ndege kutoka Kenya kutua nchini. Mashirika hayo ni Kenya Airways, AirKenya Express, Fly540 na Safarilink Aviation.

 Toa comment