Princess Dayana Humwambii Kitu kwa Mondi

1 0Princess Dayana Humwambii Kitu kwa Mondi

Mambo vipi msomaji wangu, kama ilivyo kawaida huwa tunakutana na mastaa mbalimbali Bongo na kupiga nao stori mbili tatu, ili kujua life style yao mbali na kazi wanazofanya iko vipi.

 

Leo tupo na msanii wa filamu nchini lakini pia ni prodyuza, Dayana William ‘Princess Dayana’ ambapo umaarufu wake ulianza kujulikana zaidi katika Tamthiliya ya Siri za Familia na Maisha ya Bongo.

 

Amezungumza mambo mengi usiyoyajua kutoka kwake nini anapenda na nini hapendi na kwa sababu gani, ungana nami kwa mahojiano zaidi:

My Style: Ratiba zako kwa siku huwa zikoje?

Princess Dayana: Kwanza kabisa nikiamka asubuhi lazima nisali, inategemea kama nipo kwenye diet basi nitafanya diet yangu na mara nyingi huwa naamka saa 12.

My Style: Simu yako ya kwanza kupiga huwa unampigia nani ukiamka asubuhi?

Princess Dayana: Yaani katika watu wavivu kupiga simu mimi namba moja, kwa sababu hata wazazi wangu kuwapigia simu mara nyingi huwa ni mchana siyo asubuhi.

My Style: Mtandao gani wa kijamii ambao haipiti siku haujaingia Princess Dayana: Instagram. My Style: Umeshawahi kumtaka mwanaume kimapenzi?

Princess Dayana: Hapana sijawahi. My Style: Ikitokea umependa huwa unatumia mbinu gani ili kumfikishia ujumbe?

Princess Dayana: Kwa kweli huwa sina mbinu yoyote zaidi ya kufa nalo tu moyoni, kwa sababu hata nikimuonyesha nahisi kama atanidharau.

My Style: Huwa unatumia muda gani kumkubali mwanaume pindi anapotaka kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na wewe?

Princess Dayana: (Anacheka) Inategemea, lazima nimsumbuesumbue kidogo kama mwezi mmoja mpaka miezi miwili hivi.

My Style: Unapenda marafiki wa aina gani?

Princess Dayana: Napenda marafiki wanaojitambua na wanajua wanataka nini, pia wawe na maono ya mbali.

My Style: Kitu gani ambacho hakikosekani kwenye dressing table yako?

Princess Dayana: Perfume, mafuta, lipstick na poda.

My Style: Wewe ni chizi nini?

Princess Dayana: Mimi ni chizi pochi, viatu na nguo.

My Style: Starehe yako kubwa ni nini?

Princess Dayana: Starehe yangu kubwa ni kuangalia series.

My Style: Ukiwa umetulia nyumbani huwa unapenda kufanya vitu gani?

Princess Dayana: Sanasana napenda kusikiliza muziki.

My Style: Unapenda style my mwanaume mwenye vigezo vipi?

Princess Dayana: anayejitambua na mtafutaji.

Mwanaume My Style: Umeshawahi kwenda kwa mganga? Princess Dayana: Hapana, sijawahi.

My Style: Unapenda kusikiliza muziki wa Bongo Fleva? Princess Dayana: Sana yaani.

My Style: Ikitokea kuna shoo mbili moja ya Ali Kiba na nyingine Diamond utaenda ipi?

Princess Dayana: (Anacheka) Nitaenda ya Diamond.

My Style: Kwa nini Diamond?

Princess Dayana: mtu ambaye haridhiki na mafanikio, Kwa sababu ni yaani ni mtu ambaye anaweza akakaa hata mwezi hajaachia kitu lakini akija kuachia ngoma lazima tufurahi.

My Style: Msanii gani wa kike ambaye unamuangalia kama mfano wa kuiga?

Princess Dayana: Monalisa, napenda sana life style yake.

My Style: Jambo gani ambalo hupendi kufanyiwa.

Princess Dayana: kusemwa. Sipendi My Style: Mwanaume wa aina gani hata awe mzuri na pesa kiasi gani huwezi kuwa naye kimapenzi?

Princess Dayana: Mwanaume mwenye show off za kijinga na anayeongea sana, yaani hata iweje siwezi kuwa naye.

Makala: Memorise RichardToa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *