Prof. Jay Ashindwa Ubunge

MSANII wa Bongo Fleva nchini, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay,  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameshindwa kutetea Jimbo la Mikumi, ambalo alikuwa mbunge kwa kipindi cha miaka mitano.

 

Amepata kura 17,375 huku mpinzani wake Denis Lazaro wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiibuka mshindi kwa kupata kura 31,411.

 

Mbunge huyo maarufu nchini alipata wadhfa wa ubunge wa jimbo hilo tangu mwaka 2015 baada ya kutamba na wimbo wa ‘Ndiyo mzee’ ambao ulikuwa unaeleza namna kiongozi anavyoweza kutoa ahadi bila kuzitimiza.

 

r
Toa comment