PSG Yatupa Ndoano Kwa Hector Bellerin

KLABU ya PSG imepeleka ombi la kumtaka beki wa Arsenal, Hector Bellerin baada ya beki wao Thomas Meunier kuondoka bure kuanzia mwezi Juni mwaka huu.PSG ilikuwa kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo walichapwa bao 1-0 na Bayern Munich.

 

PSG katika mchezo wa fainali walimtumia Thilo Kehrer ambaye alicheza upande wa kulia kwenye mchezo huo.Pamoja na kwamba PSG walimsajili kinda Colin Dagba, bado waliona kuwa hana uwezo wa juu sana wa kuichezea timu hiyo.

 

Juzi ilielezwa kuwa kocha wa PSG, Thomas Tuchel amemweka Bellerin kuwa beki chaguo namba moja kwenye kikosi chake.

Bellerin raia wa Hispania amekuwa kwenye kiwango cha juu sana kwenye kipindi chote ambacho ametumika kwenye kikosi cha Arsenal kuanzia mwaka 2011. Kehrer ndiye alishindwa kumzuia Kinglsey Coman, ambaye alipiga kichwa kilichozaa bao pekee kwenye mchezo huo wa fainali, Jumapili iliyopita.

 

Nahodha huyo msaidizi wa Arsenal, pia anawindwa na klabu kubwa za Ulaya; Atletico Madrid, Ju-ventus, Se-villa, Inter Milan na Bayern Munich.Hata hivyo, itakuwa ngumu kwa Bellerin kuondoka kwenye timu hiyo kwa kuwa bado ana mkataba na Arsenal hadi mwaka 2023 na amekuwa chaguo la kwanza la kocha Mikel Arteta.

MBUNGE GULAMALI Alivyoimba WIMBO wa DIAMOND Wakati AKIRUDISHA FOMU…Toa comment