R.Kelly ashambuliwa gerezani, wakili wake aomba aachiliwe

1 0

Wakili wa R. Kelly ameomba mteja wake achiliwe huru mara moja baada ya kusemekana kwamba ameshambuliwa na mfungwa mwenzake.

Steve Greenberg amesema mteja wake alishambuliwa katika kituo cha kurekebisha tabia cha Chicago, ambapo Kelly anasubiri kusikilizwa kwa kesi yake dhidi ya madai ya unyanyasaji wa kingono.

Kiwango cha majeraha bado hakijafahamika, Bwana Greenberg amesema kupitia mtandao wa Twitter.

Kelly hajapatikana na hatia kwa makosa kadhaa ikiwemo ya unyanyasaji dhidi ya watoto na biashara ya ngono.

Taarifa za madai ya kushambuliwa kwake kuliripotiwa kwa mara ya kwanza na tovuti ya habari ya TMZ, ambayo imesema kwamba mfungwa mwenzake alianza kumpiga Kelly ngumi akiwa ameketi kwenye kitanda chake.

Mfungwa huyo alikuwa na hasira kuhusu matukio ya mkuu wa gerezani kufika kwenye kituo hicho mara kadhaa kwasababu mashabiki wa Kelly wanaandana nje ya kituo hicho.

Uelewa wangu ni kwamba kila wakati kuna maandamano yanayo muunga mkono Kelly nje ya gereza, gereza lote hulazimika kufungwa,” Bwana Greenberg amesema.

Kelly, ambaye alikuwa miongoni mwa nyota maarufu wa muziki aina ya R&B miaka ya 1990, amekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja wakati akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake huku kesi zilizowasilishwa dhidi yake zikiwa Illinois, Minnesota na New York.

Amenyimwa dhamana mara tatu na hakimu wa Brooklyn alisema kuna uwezekano mkubwa ushahidi kuingiliwa katika kesi ambapo anadaiwa kuongoza kundi la uhalifu kwa muda mrefu kusajili wanawake na wasichana kufanya na mapenzi nao.

R Kelly
R Kelly alikuwa mmoja wa wanamuzi nyota mtindo wa R&B miaka ya 1990

Kesi hiyo inatarajiwa kuanza mwezi ujao lakini wakili wa Kelly ametoa wito kwa nyota huyo kuachiliwa huru kwa wakati huu kulinda usalama wake.

“Serikali haiwezi kumuhakikishia usalama wake, na haiwezi kumuachilia,” Bwana Greenberg ameandika kwa mtandao wa Twitter. “Hatustahili kufunga watu milele kwasababu hatuwezi kutoa mchakato yakinifu wa kisheria.”

Msemaji wa gereza serikalini hakuweza kuthibitisha au kukataa taarifa za kwamba Kelly ameshambuliwa.

Bwana Greenberg amesema “amepokea taarifa za kukanganya kuhusiana ukubwa wa majeraha aliyopata na kwamba hajapewa taarifa zozote kutoka gerezani”.

“Ni matumaini yetu kwamba hakupata majeraha makubwa sana,” aliongeza.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *