Rais Azuiwa Kushiriki Uchaguzi

RAIS wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo amezuiwa kugombea urais katika uchaguzi ujao baada ya mahakama kuidhinisha uamuzi wa tume ya uchaguzi.

 

Wakili wake Claude Mentenon amelimbia shirika la habari la AFP amesema kuwa kuna matatizo menginezaidi ya kisheria ndani ya Ivory coast dhidi yake. Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo ilimuondoa katika orodha ya wagombea kwasababu alipatikana na hatia ya uhalifu.

 

Rais wa tume ya uchaguzi , Ibrahime Coulibaly-Kuibiert, alisema mwezi Agosti kwamba yeyote anayepatikana na hatia ya uhalifu ataondolewa kwenye orodha ya wagombea. Alitoa tangazo hilo wakati alipokua akitangaza orodha mpya ya wagombea.

 

Wagombea wanne akiwemo kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro waliondolewa kwenye orodha ya wagombea wa urais. Gbagbo aliondolewa mashitaka mwezi Januari 2019 baada ya kushitakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu uliohusiana na ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.Toa comment