Rais JPM Amtumbua Balozi “Abebe Msaba Wake” – Video

Rais Dkt. John Magufuli amesema kuwa amemrejesha nyumbani aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, na kuwa si balozi tena. Ripoti Ya CAG mwaka 2018/19 imeeleza kuhusu upotevu/matumizi mabaya ya mabilioni ya fedha katika ubalozi huo.

 

Magufuli amesema hayo leo Alhamisi, Machi 26, 2020 wakati akihutubia baada ya kupokea Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere na Ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).

 

“Mmebaini wizi katika ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia na yule balozi nimeshamrudisha, siyo balozi tena kule. Itakuwa ni fundisho kwetu sisi kwamba ukiharibu mahala fulani ujiandae kubeba msalaba.

 

“Kwa mashirika 10 tu ya UMMA Nakupongeza CAG umeokoa Shilingi bilioni 1.2 nakupongeza sana haiwezekani kazi yetu wenyewe tukaguliwe na watu wengine,” amesema Rais Magufuli.

 

Awali akiwasilia ripoti hiyo kwa Rais Magufuli, CAG Kichere amesema katika ukaguzi wake unaoishia Juni 30, 2019 amebaini Balozi za Tanzania nchini Brazil, Nigeria na Stockholm/Sweden zimetumia Sh1.02 bilioni kukodi nyumba za makazi.

 

Kichere ameyasema hayo leo Machi 26, jijini Dodoma wakati akiwasilisha ripoti yake kwa Rais John Magufuli ya ukaguzi wa mwaka 2018/19. Kichere amesema kiasi hicho cha fedha kingeweza kuepukika kama balozi hizo zingekarabati nyumba zao za makazi.

 

Pia, Kichere amesema katika ukaguzi wake amebaini kwamba balozi 14 za Tanzania zina majengo ambayo yametelekezwa, hivyo ameshauri majengo hayo kukarabatiwa ili kuokoa fedha ambazo zinatumika kukodi nyumba. Amezitaja baadhi ya balozi hizo kuwa ni pamoja na Canada, Burundi, Kenya, Sweden na Algeria.

 
Toa comment