Rais Magufuli Apokea Ripoti Ya CAG, Ikulu Chamwino, Dodoma (Picha +Video)

14 0

Rais Magufuli Apokea Ripoti Ya CAG, Ikulu Chamwino, Dodoma (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Magufuli leo Machi 26, 2020 amekabidhiwa Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2018/2019 iliyowasilishwa na Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Seriakali (CAG) Charles Kichere, Aidha Mhe.

 

Rais amepokea Ripoti ya taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2018/2019 itakayowasilishwa na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Taasisi hiyo Brigedia Jenerali John Mbungo . Hafla inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ikulu Chamwino Jijini Dodoma Machi 26, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ripoti ya Mwaka 2018-2019 kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 26/03/2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisoma Muhtasari wa Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ya Mwaka 2018-2019 iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 26/03/2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Makabrasha ya Taarifa Mbalimbali alizokabidhiwa na CAG katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ripoti ya Mwaka 2018-2019 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea Ripoti mbili za Mwaka 2018/19, moja kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo akisoma Muhtasari wa Taarifa yake ya Mwaka 2018-2019 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshika Taarifa ya Mwaka 2018/2019 ya CAG pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi mara baada ya kuwakabidhi pamoja na Taarifa ya TAKUKURU kwa ajili ya kuzifanyia kazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kutoka kwenye ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo alipokea Ripoti mbili za Mwaka 2018/2019 kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa PCCB pamoja na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu, pamoja Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakitoka kwenye ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

PICHA NA IKULU
Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *