Rais Magufuli Awashukuru Viongozi wa Dini Kwa Kuomba dhidi ya Corona

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati alipokuwa akiendesha Harambee ya Papo kwa papo kwa ajili ya upanuzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Bikira Maria Imaculata Chamwino Ikulu mkoani Dodoma leo tarehe 7 Juni 2020. Katika Harambee hiyo jumla ya Shilingi Milioni 17 zilipatikana pamoja na mifuko 76 ya Saruji na Mhe. Rais Magufuli alichanga peke yake kiasi cha Shilingi Milioni 10.

Rais Magufuli leo Juni 7, 2020 amewashukuru Viongozi wa Dini na Watanzania wote kwa kuitikia wito wa kumuomba Mwenyezi Mungu aepushe janga la ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19).Toa comment