Rais Magufuli Azindua Safari za Ndege Kutoka Dar – Mpanda (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli  leo Jumamosi Oktoba 12, 2019 amezindua safari za Shirika la ndege la Tanzania ATCL kutoka Dar kwenda Mpanda mkoani Katavi.

Rais Magufuli amesema hadi leo Jumamosi watu 138 waliokuwa wakidaiwa kuwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kuomba msamaha kwa DPP, wamerudisha fedha, wametubu na kuachiwa.

Amesema “Walioachiwa wako huru wamekwenda kujumuika na familia zao. Huo ndiyo upendo wa pekee kwa sababu tulitoa msamaha na wao wamepokea na sisi tunashukuru. Hao sasa ni raia wema wahesabike kuwa ni raia wema katika nchi yetu.”

Aidha, ameongeza kuwa kulikuwa na watuhumiwa 700 walioomba msamaha na wataendelea kuachiwa kadri watakavyo rudisha fedha na fedha hizo zitatumika katika shughuli za maendeleo ya Watanzania

Toa comment