Rais mpya Mali kuapishwa leo

10 0

Rais mpya wa Mali ataapishwa leo ikiwa ni wiki tano baada ya kuondolewa madarakani kwa Boubacar Keita.

Waziri wa ulinzi wa zamani, Bah Ndaw ameteuliwa na kiongozi wa jeshi, kanali Assimi Goita, ili kuongoza kwa mpito mpaka uchaguzi utakapofanyika.

Wakati Kanali Goita atakuwa makamu wa rais.

Serikali mpya inatarajiwa kuwa madarakani kwa kipindi cha mpito cha miezi 18, kipindi ambacho uchaguzi utakapofanyika.

Kuteuliwa kwa rais ambaye ni raia, lilikuwa sharti la kundi la mataifa ya Afrika Magharibi, Ecowas, ili kuondoa zuio waliloliweka katika nchi hiyo baada ya mapinduzi.

Bidhaa zimeanza kupatikana kwa shida katika mji mkuu wa Bamako, ingawa wanatarajiwa tangazo kutoka Ecowas baada ya uteuzi huu kukamilika.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *