Rais wa Brazil Jair Bolsonaro ajiunga na waandamanaji kupinga amri ya kubaki nyumbani kisa Corona

17 0

Hapo jana Rais Jair Bolsonaro wa Brazil alijiunga na mamia ya waandamanaji nje ya makao makuu ya jeshi mjini Brasilia kupinga amri ya kubakia nyumbani iliyotangazwa na magavana wa majimbo nchini humo.

Rais Bolsonaro aliwaambia waandamanaji kuwa amejiunga pamoja nao kwa sababu anakubaliana na mawazo wanayotoa. Hata hivyo taifa hilo la Brazil linaidadi kubwa ya maambukizi katika eneo la Amerika ya Kusini.

Mara kadhaa kiongozi huyo amekosoa hatua zilizochukuliwa na magavana za kuweka vizuizi vya wastani ikiwemo kwenye miji yenye idadi kubwa ya watu ya Sao Paulo na Rio de Janeiro ili kuzuia kusambaa virusi vya corona.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *