Rais wa Israel amtaka Waziri Mkuu Netanyahu kuunda serikali ya muungano, mpinzani wake agoma adai hatoshiriki 

6 0

Rais wa Israel amtaka Waziri Mkuu Netanyahu kuunda serikali ya muungano, mpinzani wake agoma adai hatoshiriki

Rais wa Israel, Reuven Rivlin

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Voice of America (VOA), Rais wa Israel Reuven Rivlin amemtaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kujaribu kuunda serikali mpya ya muungano baada ya uchaguzi wa wiki iliyopita kutopatikana mshindi wa moja kwa moja na hivyo umezorotesha maendeleo ya nchi.

Ofisi ya Rais Reuven Rivlin ilitoa tangazo baada ya kukutana Jumatano na Netanyahu pamoja na mpinzani wake wa karibu Benny Gantz.

Rais Rivlin anajukumu la kumchagua mgombea anayeamini kwamba ana fursa kubwa ya kuunda serikali ya umoja baada ya wote Netanyahu wala Gantz kutopata uungaji mkono unaohitajika kwa kupata wingi wa viti katika bunge la israel.

Image result for Benjamin Netanyahu vs Benny Gantz

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu (kushoto) Benny Gantz (kulia).

Rivlin aliongoza mikutano miwili ya awali wiki hii kati ya wanasiasa hao akitumaini kufikia makubaliano kati ya chama cha kikonservative cha Netanyahu cha Likud na ushirika wa mrengo wa kati na wastani wa Blue and White unaoongozwa na Gantz.

Mazungumzo yalimalizika bila kupata suluhisho juu ya nani anatakiwa kuongoza serikali mpya ya umoja. Gantz anasema hatoshiriki katika serikali inayoongozwa na Netanyahu kwa sababu ya matatizo ya kisheria yanayomkabili Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Netanyahu anania ya kuendelea kubaki madarakani kama Waziri Mkuu licha ya uchunguzi wa rushwa unaoendelea dhidi yake.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *