Rayvanny Afungukia Kuficha Uhusiano Mpya!

STAA wa Bongo Fleva na memba wa Lebo kya Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, amefunguka sababu ya kuficha uhusiano wake mpya.

 

Rayvanny ameiambia OVER ZE WEEKEND kuwa, kuweka uhusiano hadharani ni uamuzi wa mtu mwenyewe.

 

“Hakuna binadamu ambaye anakosa uhusiano, lakini kuweka hadharani au kutokuweka ni uamuzi wa mtu. Ninachojua mpenzi ni wako sasa unavyoweka mtandaoni watu wanaona kila kitu, wapo ambao wataanza kurusha mishale yao, hapo unabaki kujiuliza mpenzi wako atakwepa mishale yote?’’

 

Anasema Rayvanny ambaye hivi karibuni ameachana na mzazi mwenzake, mwanamitindo na mjasiriamali, Fahyma Msenga ‘Fahyvanny’ aliyezaa naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Jaydanny.

 

 STORI: HAPPYNESS MASUNGAToa comment