Rayvanny Amkana Fahy Vanny Kweupee

BAADA ya stori nyingi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mrembo Fahima MsengaFahyvanny” amerudiana na mzazi mwenziye, msanii kutoka katika lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond MwakyusaRayvanny’ na kwa sasa wanaishi pamoja, msanii huyo ameibuka na kuanika ukweli.

 

Rayvanny alipoulizwa kuhusu tetesi hizo, alikanusha kwa kifupi na kukata simu. “Nani kasema tumerudiana?”

 

Hilo ndilo jibu fupi kutoka kwake Rayvanny ambaye sasa anatamba na ngoma yake ya Corona, wimbo ambao unafundisha watu jinsi ya kujilinda na maambukizi ya virusi hivyo.
Toa comment