Rayvanny Aombwa Kugombea Ubunge 2020

STAA wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ anayetumikia Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), amefunguka juu ya ishu ya kuombwa kugombea ubunge mwaka huu kwenye Uchaguzi Mkuu 2020 huko nyumbani kwao jijini Mbeya.

 

Rayvanny au Van Boy ameiambia OVER ZE WEEKEND kuwa, ishu hiyo ilitokea alipokwenda nyumbani kwao, Nzovwe (Jimbo la Mbeya-Mjini), lakini kwa upande wake bado hajawaza kugombea.

 

“Kuna kipindi nilikwenda Mbeya, watu wakaniomba nichukue fomu ya kugombea, ila mimi kwa sasa niko bize na muziki wangu maana ni kitu ambacho ninakiweza zaidi,’’ amesema Rayvanny.

 

OVER ZE WEEKEND inafahamu kwamba Jimbo la Mbeya- Mjini lipo chini ya Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na litakuwa na ushindani mkubwa kwenye uchaguzi wa Oktoba, mwaka huu.

STORI: HAPPYNESS MASUNGA
Toa comment