RC Kunenge Afanya Ziara ya Kushtukiza Usiku Atoa Maagizo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amefanya ziara ya kustukiza Usiku wa manane kwenye miradi mitatu mikubwa ikiwemo ya Ujenzi wa Machinjio ya kisasa Vingunguti, Soko la Kisutu na ujenzi wa Stendi ya kisasa Mbezi Louis kujionea Kama agizo alilotoa la kufanya kazi usiku na Mchana linatekelezwa.

 

Akiwa kwenye ujenzi wa Machinjio ya kisasa Vingunguti na Soko la Kisutu RC Kunenge amekuta agizo la kufanya kazi usiku na Mchana halijatekelezwa jambo linalopelekea Miradi hiyo kushindwa kukamilika ndani muda uliopangwa na kuleta kero kwa wananchi.

 

Kutokana ukiukwaji wa maagizo yayo RC Kunenge ametoa maagizo matatu mazito kwa Manispaa ya Ilala ikiwemo kuhakikisha Mkandarasi anapigwa faini kwa kushindwa kukamilisha ujenzi ndani ya muda kwa mujibu wa mkataba, Kumchukulia hatua za kinidhamu Msimamizi wa Mradi pamoja na kumuwajibisha Mhandisi Manispaa hiyo kwa kushindwa kusimamia kazi yake.
Toa comment