RC Kunenge aridhishwa na hatua za utekelezaji wa maagizo aliyotoa Rais Magufuli juu ya miradi Dar Es Salaam

17 0

Utekelezaji wa maagizo mbalimbali ya ujenzi wa Miradi ya maendeleo jijini Dar es salaam yaliyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli yametekelezwa kwa asilimia kubwa ambapo leo Mkuu Wa Mkoa huo Mhe. Aboubakar Kunenge amefanya ziara ya kukagua utekelezaji Wa maagizo hayo na kuonyesha kuridhishwa na hatua miradi ilipofikia.

Miongoni mwa miradi aliyotembelea RC Kunenge ni mradi mkubwa wa ujenzi wa machinjio ya kisasa ya Vingunguti ambapo amesema ifikapo Jumapili machinjio hayo yataanza majaribio ya kwanza ya uchinjaji Wa Mbuzi na kueleza kuwa kabla ya November 20 zoezi la kufunga mashine litakuwa limekamilika.

Aidha RC Kunenge ametembelea mradi Wa ujenzi Wa nyumba 24 za Watumishi Wilaya ya Kigamboni ambazo Rais Magufuli alitoa kiasi cha shilingi Bilioni 2 kwaajili ya kuhakikisha watumishi wanakuwa na makazi bora ambapo ujenzi unaendelea vizuri na unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi November.

Akiwa Wilaya ya Kigamboni RC Kunenge ametembelea ujenzi Wa Barabara yenye urefu wa Km 2 kutoka Daraja la Mwalimu Nyerere pamoja na ujenzi Wa Round about ya kuunganisha kibada, Feri na barabara ya kuelekea darajani ambavyo vyote vimekamilika.

Pamoja na hayo RC Kunenge ametembelea ujenzi wa Barabara ya Kinondoni Shamba ambayo Rais Dkt. John Magufuli aliagiza barabara hiyo itengenezwe baada ya wakazi Wa maeneo hayo kutoa malalamiko na sasa jambo jema ni kwamba ujenzi Wa barabara hiyo umekamilika kwa 100%.

Katika hatua nyingine RC Kunenge ameridhishwa na utekelezaji Wa agizo la Rais la kutaka wafanyabiashara wadogowadogo waliokuwa stand ya mbezi wajengewe soko la kisasa ambapo tayari manispaa ya ubungo ipo hatua ya mwisho kukamilisha ujenzi Wa soko hilo lenye uwezo Wa kubeba wafanyabiashara 552.

DAR ES SALAAM TUNATEKELEZA KWA VITENDO.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *