RC Mwanri Ataka Wananchi Kususia Maduka Yasiyo na Sanitizer – Video

MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa huo kutoa taarifa za wageni wasiofahamika walikopotoka pindi wanaonekana katika maeneo yao ili kuepuka kuambukizwa homa kali ya mapafu inayoenezwa na kirusi kipya aina ya Corona.

 

Alisema Mkoa huo ni mkubwa na unapatakana na mikoa inayopakana na Nchi za jirani na upo uwezekano wa wageni kuingia kwa kutumia njia za panya na hivyo kuhatarisha afya za wakazi wa Tabora.

 

Mwanri alitoa kauli hiyo leo wakati alipokuwa akifungua mkutano wa timu ya Mkoa wa Tabora ya kudhibiti janga la Corona lisiingie mkoani humo.

 

Aliwahimiza wananchi kuendelea kuchuka taadhari dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayoenezwa na kirusi kipya aina ya Korona kwa kunawa mikono mara kwa mara.

 

Aidha Mwanri aliwataka wananchi kususia maduka yote ambayo wamiliki wake watakutwa hawaweka vitakasa mikono ama ndoo kwa ajili ya wateja kunawa kabla ya kununua bidhaa.

 

Mwanri alisema wamiliki wa aina hiyo wana nia mbaya na Watanzania na wanapingana na maagizo ya viongozi wa Kitaifa na wataalamu ya kuwataka wananchi kuna mikono kama kinga ya janga la Corona.

 

Amevitaka vyombo vya habari na Redio zilizomo mkoani humo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na janga la corona ili Mkoa huo uendelee kuwa salama.

 
Toa comment