Rihanna: Chris Brown ni Mpenzi wa Maisha Yangu

WAKATI watu wengi wakidhani kwamba uhusiano wao ulikufa mwaka 2009  baada ya Chris Brown ‘Breezy’ kumpa kipigo mrembo aliyekuwa mpenzi wake, Rihanna, kisha kufikishana mahakamani na kutengana, kwenye mahojiano na Oprah Winfrey kupitia Podcast yake “Supersoul Conversation” Riri amesema bado wanapendana sana na daima wataendelea kuwa marafiki wa karibu.

 

“Tumeendelea na urafiki wetu tena, kwa sasa sisi ni marafiki wa karibu sana. Tumerudisha uaminifu tena, kwa hivyo tunapendana sana tutafanya hivyo kila siku. Na hicho si kitu ambacho kitaenda kubadilika, hicho si kitu ambacho unaweza kukizima au kukiepuka, kama ulishawahi kuwa kwenye mapenzi.” amesema Rihanna.

 

Rihanna hakuishia hapo, aliendelea kwa kusema: “Nafikiri alikuwa mpenzi wa maisha yangu. Alikuwa mpenzi wangu wa kwanza. Na ninaona ananipenda kama mimi ninavyompenda, wala si kwamba eti tutakuwa pamoja. Ninampenda sana. Kitu kikubwa kwangu ni kwamba ana amani. Mimi sitakuwa na amani kama yeye atakuwa hana furaha hata kidogo, au akibaki mpweke,” alikazia Riri.Toa comment