Rodriguez Asaini Miaka Miwili Everton

TIMU ya Everton imemtangaza mshambuliaji mpya James Rodriguez ambaye imemsajili kwa kitita cha pauni milioni 20.

 

Staa huyo ambaye alikosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Real Madrid kwa muda mrefu anakwenda kukutana na kocha wake wa zamani Carlo Ancelotti.

 

Everton wanaamini kuwa staa huyo raia wa Colombia anaweza kuisaidia timu hiyo kufanya mambo makubwa sana kwenye Ligi Kuu England msimu ujao.

James Rodriguez

James amesaini mkataba wa miaka miwili na timu hiyo, lakini ukiwa na kipengele cha kuongeza mkataba mwingine wa mwaka mmoja.

 

Ancelotti amekuwa akimfahamu zaidi staa huyo kwa kuwa alimfundisha kwenye kikosi cha Real Madrid na Bayern Munich.Toa comment