Ronaldinho Aachiliwa Huru Paraguay

 

MCHEAJI wa soka wa Brazil,  Ronaldinho,  ameachiliwa kutoka kifungo cha nyumbani nchini Paraguay baada ya kufungwa kwa kumiliki paspoti ya kugushi.

 

Mwezi Machi yeye na kaka yake walidaiwa kutumia paspoti feki kuingia nchini Paraguay.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia na kaka yake wamekuwa gerezani kwa mwezi mmoja na miezi mingine minne ambapo alifungiwa katika hoteli ya kifahari iliyopo katika mji mkuu wa Asuncion kwa dhamana.Toa comment