Rose Muhando Waimba Injili Wenzake Kukiwasha Kuombea Uchaguzi

Mkongwe wa uimbaji nyimbo za injili nchini, Rose Muhando anatarajiwa kuwaongoza waimba injili wenzake katika tamasha la kuombea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Septemba 6 mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, muandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama amesema tamasha hilo lilipaswa kufanyika Agosti 23 lakini wameliahirisha na kufanyika siku hiyo.

“Kutokana na shughuli za kimichezo zinazoendelea zimesababisha kupelekwa mbele kwa tamasha hili lakini waimbaji wataimba kama walivyopangiwa”. Amesema Msama.

Kwa upande wake, Rose Muhando amesema ana imani waimbaji wote wamejipanga vizuri kwa ajili ya kuimba kwenye tamasha hilo.

“Hatujawahi kupoa na hatupoi siku hiyo tutawasha moto uwanja wa Uhuru kuombea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Kwakuwa mungu wetu hajawahi kupoa hivyo tunatarajia kuwasha moto usiozimika Watanzania msipange kukosa.” Alimaliza kusema Rose.

HABARI/PICHA NA MWANDISHI WETUToa comment