Rotimi wa Vanessa Mdee Aanza Kujifua Kiswahili

MPENZI wa msanii, Vanessa Mdee Rotimi, ameonekana akijifunza kuongea lugha ya Kiswahili ambapo alikuwa anafundishwa baadhi ya maneno na mpenzi wake huyo.

 

Rotimi ameonekana akifundishwa kutamka maneno hayo kupitia Insta Story ya Vanessa Mdee ambapo alikuwa anamwambia ataje maneno ya Kiswahili kama yafuatayo.

 

“Ahh Mama yangu, jamaani kabisa polee,” amesema  Rotimi.

 

Wawili hao wanakaribia kumaliza mwaka sasa tangu walipoanza mahusiano yao mwaka 2019, ambapo Vanessa  alikuwa ametoka kuachana na msanii wa RnB, Juma Jux.

 Toa comment