RPC Dodoma Aelezea Mbowe Kuvamiwa na Kuvunjwa Mguu

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amevamiwa na watu watatu waliomkanyaga na kumvunja mguu wake wa kulia.

 

Hayo ameyabainisha mapema leo Juni 9, 2020, na kusema kuwa taarifa kamili wataitoa hapo baadaye.

 

“Ni kweli, zipo taarifa kuwa Mhe. Freeman Mbowe amevamiwa na watu watatu wakamkanyaga kanyaga na kumvunja mguu wa kulia kwa sasa yuko Ntyuka wodi no 4 na anaendelea vizuri, bado tunaendelea kuchunguza tutawajulisha baadaye,” – Gilles Muroto, RPC Dodoma.

 

Imeelezwa kuwa Mbowe ameshambuliwa majira ya saa 7:00 usiku wa kuamkia leo.Toa comment