Samia Suluhu Alivyofanya Kampeni Dar, Ataja Miradi Itakayotekelezwa 2020,25

1 0Samia Suluhu Alivyofanya Kampeni Dar, Ataja Miradi Itakayotekelezwa 2020,25

Makamu wa Rais,Samia Suluhu (katikati) akiwa meza kuu kabla ya kuhutubia wananchi wa maeneo ya Tabata Shule.

Maelfu ya wakazi wa Dar waliojitokeza kusikiliza sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) viwanja vya Tabata shule.

Baadhi ya wanachama wa CCM wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.

Sehemu ya Baadhi ya wasanii wanaokiunga mkono Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Maelfu ya wakazi wa Dar waliojitokeza kusikiliza sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) viwanja vya Tabata shule.

Msaga Sumu akitoa burudani ya aina yake katika viwanja vya Tabata shule jijini Dar es Salaam katika ziara ya Makamu wa Rais Samiah Suluhu ya Kampeni ya kumnadi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akizungumza  wakati wa mkutano wa Kampeni uliofanyika Tabata shule Jijini Dar es Salaam,amesema kuwa.

“Ndugu zangu tunatambua changamoto za miundombinu kwenye Jiji hili, na ndio maana tunajenga Barabara za juu, madaraja na mifereji, Daraja la Salenda linaendelea vizuri, interchange ya ubungo tunakaribia kumaliza na tumetenga fedha zaidi ya bilioni 32 za mifereji ili kuzuia mafuriko”alisema Samia.

“Tumejenga machinjio ya kisasa ya vingunguti ambayo huiingizia Serikali pato la zaidi ya sh. Milioni 100 kwa mwezi, alisema tayari zimetengwa shilingi Bilioni 12.49 ambapo hadi kufikia Septemba 30, mashine za kisasa za uchinjaji zitakuwa zimefungwa.

Kwenye suala la elimu Mh.Samia alisema kuwa wametenga takribani shilingi Bilioni 44.5 kuboresha sekta hiyo kwa kujenga madarasa, ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

Amesema pia uboreshaji wa miundombinu katika sekta ya utalii Jiji hilo litajenga ukumbi mkubwa  wa kisasa wa kitalii ambao utajumuisha hoteli, huku mikakati ya kutengeneza gati kwa ajili meli kubwa za kitalii ikifanywa.

Aidha pia alisema Serikali inaendelea kuboresha ukusanyaji wa mapato yatokanayo na utalii.

 

 

 Toa comment

Posted from

Related Post

Ed Sheeran Atangaza Kupumzika Muziki

Posted by - August 29, 2019 0
Ed Sheeran Atangaza Kupumzika Muziki August 29, 2019 by Global Publishers MWANAMUZIKI maarufu duniani, Mwingereza, Edward Christopher Sheeran,  maarufu kama…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *