Sancho aziingiza vitani Man Utd, Man City

22 0


MANCHESTER, ENGLAND

KLABU hasimu kutoka jiji moja Manchester United na
Manchester City, zimeingia vitani kuwania saini ya kinda wa kimataifa wa
England, Jadon Sancho anayekipiga katika kikosi cha Borussia Dortmund ambaye
ameonyesha wazi kuwa anataka kuondoka kwa miamba hiyo ya nchini Ujerumani.

Dortmund tayari wameanza kusaka mbadala wa nyota huyo wa kimataifa
wa England mara baada ya kukubali kumuachia akatafute changamoto mahala
pengine.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, klabu yoyote inayotaka
saini ya kinda huyo inapaswa kutoa dau nono huku thamani yake ikiwa pauni
milioni 100.

City wanamuangalia kwa ukaribu zaidi kinda huyo ambaye
ambaye alikulia katika kikosi hicho kabla ya kumuuza kwa dau la pauni milioni 7
mwaka 2017.

Klabu hizo zinatarajia kuonyeshana umwamba ili kumnasa
kinara huyo wa pasi za mwisho nchini Ujerumani ambaye alimaliza akiwa ametoa
jumla ya pasi 14.


Source link

Related Post

Jembe la Yanga Lasaini Azam FC

Posted by - July 25, 2020 0
Jembe la Yanga Lasaini Azam FC July 25, 2020 by Global Publishers INAELEZWA kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mohammed Issa ‘Mo…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *