Sarpong, Carlinho Wtupia Mazoezini Yanga

1 0Sarpong, Carlinho Wtupia Mazoezini Yanga

AMA kweli Yanga inautaka ubingwa msimu ujao, hiyo ni baada ya kuukosa kwa misimu mitatu mfululizo jambo ambalo limefanya safari hii kurudi kivingine kwa kupiga tizi la maana katika maandalizi ya msimu ujao wa 2020/21.

 

Yanga imeendelea na mazoezi yake katika Uwanja wa Chuo cha Sheria uliopo Ubungo Mawasiliano jijini Dar, huku wakishuhudia nyota wake wote wapya waliotua hivi karibuni nchini wakiwa mazoezini.

 

Katika mazoezi hayo yanaoendelea kusimamiwa na Kocha Msaidizi, Juma Mwambusi, yalionekana kufuatwa kwa weledi na wachezaji wa kikosi hicho.

Mwambusi katika mazoezi ya jana alionekana kuunganisha timu na kuifanya icheze soka la pasi na kuwapa mbinu mbalimbali za kufunga mabao hususan kwa viungo na washambuliaji wa timu hiyo.Walianza na mazoezi kwa kukimbia, pia wakiingia zoezi kukaba na kutoa pasi ili kuwaweka fiti wachezaji.

 

Kisha likaingia lile la kufunga mabao ambapo walioonekana kufaya vizuri walikuwa ni washambuliaji Mghana, Michael Sarpong na Muangola, Carlos Carlinho ambao kila mmoja alicheka na nyavu.

 

Katika mazoezi ya timu hiyo Sarpong alifanikiwa kufunga mabao matano huku Carlinhos akifunga mabao matatu sawa na Tuisila Kisinda raia wa DR Congo na Waziri Junior akifunga mawili.

Baadaye Championililishuhudia kocha Mwambusi akizigawa timu mbili tofauti ambazo zilicheza mechi iliyomalizika kwa sare ya mabao 1-1 ambapo Ditram Nchimbi na Michael Sarpong walitupia.

 

VIKOSI VYA TIMU HIZOKIKOSI A: Metacha Mnata, Paul Godfrey, Adeyum Saleh, Said Makapu, Abdulaziz Makame, Zawadi Mauya, Juma Mahadhi, Haruna Niyonzima, Ditram Nchimbi, Carlos Carlinhos na Farid MussaKIKOSI B: Farouk Shikhalo, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu, Mukoko Tonombe, Deus Kaseke, Feisal Salum, Michael Sarpong, Wazir Junior na Tuisila Kisinda.

Akizungumza na Championi Jumamosi mara baada ya mazoezi hayo, Mwambusi alisema kuwa anatarajia kuona timu ikifanya vizuri kwa msimu unaokuja kutokana na ubora wa wachezaji ambao wamesajiliwa ndani ya kikosi hicho ila wanahitaji muda ili kuwa fiti kutokana na wengi kutokuwa na mazoezi huko walikotoka.

 

“Kikosi kipo vizuri, natarajia kuona wachezaji wakifanya vizuri kwa kuwa utaona usajili uliofanyika ni mzuri hivyo ukiunganisha na wachezaji wa hapa nyumbani utaona kuwa tuna timu nzuri, lakini baadhi ya wachezaji ambao ni wakimataifa wanahitaji muda kidogo ili kuwa fiti kwa kuwa wametoka katika nchi ambazo walikuwa hawachezi mpira kwa sababu ya janga la Corona,” alisema kocha huyo.

 

KUHUSU LAMINE MORO

Wakati huohuo, beki wa kati wa Yanga, Mghana, Lamine Moro jana alishindwa kufanya mzoezi na timu hiyo ikiwa ni siku ya pili mfululizo kutokana na kusumbuliwa na goti.“Nimepata matatizo kidogo na goti langu lakini sidhani kama litachukua muda kupona, natamani kucheza mchezo wa Jumapili (kesho) dhidi ya Aigle Noir lakini hiyo ni kazi ya mwalimu ila akinipanga naona kuwa naweza kucheza,” alisema Lamine.

Waandishi WETu, Dar es Salaam

 Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *