Shambulio Burundi: Watu 15 Wauawa

Takriban watu 15 wameripotiwa kuuawa na wakati watu wenye silaha walipofanya mashambulio Kusini mwa Burundi.

 

Mapigano hayo yaliyotokea katika wilaya ya Bugarama katika mkoa wa Rumonge yalianza Jumapili na kuendela hadi Jumatatu, yamewalazimisha watu kuzikimbia nyumba zao na kujificha kwenye misitu na vichakani.

 

Katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii kundi la waasi lenye makao yake katika nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo lilisema kuwa ndilo lililofanya shambulio hilo.

 

Afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Burndi amesema kuwa kuna uwezekano kwamba ghasia hizo zina uhusiano na kurejeshwa nyumbani kwa wakimbizi wa Burundi waliokimbilia Rwanda wakitoroka ghasia nchini mwao mwaka 2017.

Chanzo: www.reuters.comToa comment