Shamsa Ford ‘Amfokea’ Aunty Rundo la Wanaume

MSANII wa filamu za Bongo, Shamsa Ford ameeleza kushangazwa na kusikitishwa kwake kutokana na kile alichokidai kuwa msanii mwenzake Aunt Ezekiel anaijingiza kimapenzi na wanaume wadogo ambao kiumri haendani nao.

 

Shamsa ameyasema hayo kupitia Kipindi cha Mashamsham cha Wasafi FM ambapo amesema kuwa wanaume anaotoka nao Aunty ni wadogo sana na wanatakiwa wamuite Mwalimu Mkuu.

 

“Wale anao-date nao Aunty alitakiwa afungue shule ya Nursery School, mfano Kusah ana miaka 21, angetakiwa amuite Aunty ‘Mwalimu Mkuu. Yani huyu mwanamke, ametoka kuachana na Mose Iyobo, sina uhakika kama mimba aliyonayo ni ya mpenzi wake wa sasa, Kusah ama ni ya Mose au ya “Ssponsa” ninayemfahamu,” amesema Shamsa.

 Toa comment