Shigongo Ajiachia na Wazee wa Buchosa

14 0Shigongo Ajiachia na Wazee wa Buchosa

 

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo,  amejumuika na wazee wa Kijiji cha Nyehunge baada ya kuwakuta wakinywa pombe ya kienyeji aina ya kidugugu ambayo ni maarufu katika maeneo hayo.


Shigongo ambaye yupo kwenye kampeni za kusaka kura za ubunge wa Buchosa pamoja na kumpigia kampeni mgombea urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli  na kura za madiwani kupitia chama hicho, amekutana na wazee hao Septemba 19, 2020, na kujumika nao katika ‘kikao’ chao huku akibadilishana nao mawazo na kumweleza changamoto zilizopo katika eneo hilo ili akichaguliwa azifikishe bungeni.

Akizungumza nao wakati wa ‘kikao’ hicho, Shigongo amewaomba wazee hao kuhakikisha wanakipigia kura Chama Cha Mapinduzi ili kiendelee kuwaletea maendeleo chanya na kuboresha maisha yao kwa miaka mingine mitano ijayo.

 

“Msijaribu kuwapigia kura wapinzani, hawa kazi yao kubwa ni kupinga kila kitu, wanapinga maendeleo, wanapinga kila linalofanywa na rais wetu.  Tunafahamu tunazo changamoto nyingi katika maeneo yetu, lakini mkiichagua CCM, itaendelea kuboresha kila sekta ambayo bado ina shida.

“Tumeona kwa miaka mitano ambavyo Mheshimiwa Rais Magufuli na serikali yake wamefanya kazi kubwa ya kutuletea maendeleo, hiyo ilikuwa rasharasha tu.  Ninaomba mwendelee kutuamini, mtupatie ridhaa tukafanye makubwa zaidi na zaidi,” alisema Shigongo.

 

 

Aidha, wakizungumza na Shigongo, wazee hao walimhakikishia kuwa wananchi wa Buchosa kama kawaida yao miaka yote hawajawahi kukipa kura chama kingine, hivyo wataendeleza msimamo wao wa kuichagua CCM kwa maendeleo ya kweli.

 

“Sisi hatuchagui porojo wala longolongo, tunachagua watu wanaofanya kazi, hatutaki mageuzi, Mheshimiwa Rais ameonyesha nia ya dhati ya kuinua uchumi wetu, ametuletea barabara ya lami Sengerema hadi Nyehunge ambayo ameagiza ianze kujengwa kabla ya kuisha kwa Desemba.  Kwa nini tumuangushe Mheshimiwa Magufuli? Hatuwezi; tutamchagua Magufuli, Shigongo na madiwani 21 wa CCM, Buchosa,” alisema Mzee Mihayo.

 

Shigongo anatarajia kuzindua rasmi kampeni zake Ijumaa ijayo ya Septemba 25, 2020, katika Viwanja wa mpira vya Nyakaliro ambapo uzinduzi huo utaongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa.Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *