Shigongo: Kura Magufuli Zitavunja Rekodi Oktoba 28 – Video

2 0Shigongo: Kura Magufuli Zitavunja Rekodi Oktoba 28 – Video

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Buchosa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo James amewaomba Watanzania wote kujitokeza siku ya uchaguzi mkuu, Oktoba 28, 2020 na kumpigia kura za NIDYO mgombea urais wa Chama hicho Dkt. John Pombe Magufuli ili apate ushindi wa kishindo na akaendelee kuifanya kazi kubwa aliyoianzisha miaka mitano iliyopita ya kuletea maendeleo thabiti nchi yetu.

 

Shigongo amesema hayo asubuhi hii ya leo, Septemba 7, 2020, wakati akihutubia wananchi wa Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba kwenye Kampeni za Rais Dkt. John Pombe Magufuli huku akiwasisitiza wampe ridhaa ya kuiongoza Tanzania kwa miaka mingine mitano.

 

“Nawaomba Oktoba 28, mkafanye uamuzi wa kuchagua vitendo si porojo, sote tumeona nchi nzima inajengwa, kwa miaka mitano Tanzania imeabadilika kwa sababu ya uongozi wa Rais Magufuli, ni mwaminifu, mcha Mungu, mchapa kazi, anayejali maslahi ya wanyonge.

 

“Nchi yetu sasa ipo uchumi wa kati, mnadhani tukimuongeza miaka mitano tutakuwa wapi? Ninawaomba tuendelee kumuamini Magufuli, tuwaamini wagombea ubunge wa CCM, wagombea udiwani wa CCM, tuwape kura za kutosha za NDIYO ili Tanzania iendelee kusonga mbele.

 

“Tunataka tuvunje rekodi ya kura ambazo hazijawahi kutokea nchini tangu Uhuru, wananchi wote tumpigie kura za NDIYO mgombea Urais wa CCM, Dkt. Magufuli ashinde kwa kishindo, ili akaendelee kuijenga Tanzania mpya.

 

“Wananchi wa Buchosa mmeniamini na kunituma nikawe mtumwa wenu, nimejifunza kwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mtumishi wa Umma ni utumwa, nimeamua kuwa mtumwa wenu kwa miaka mitano, nitawatumikia kwa uaminifu, hekima na karama zote ambazo Mungu amenipa.

 

“Mambo mengi yamefanyika Buchosa, ujenzi wa Hospitali kubwa ya Wilaya, vituo vya afya, kwa sasa upasuaji unafanyika Buchosa hakuna haja ya kwenda Hospitali ya Wilaya Sengerema. Niwaombe Wana-Buchosa na Watanzania wote, tufanye maamuzi sahihi, tusifanye majaribio, tusiingize kwenye madaraka watu wasio waaminifu.” – Eric Shigongo, Mgombea Ubunge – Buchosa.Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *