Shilole Acharuka, Kisa………!

 

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva pia mjasiriamali maarufu, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amewacharukia wanaomsengenya kisa kutomzalia mumewe Ashraf Uchebe.

Akichonga na Amani, Shilole aliwataka wanaomsengenya kuachana na kuingilia maisha ya watu kwani suala hilo la mtoto haliwahusu na wakati ukifika atazaa tu.

“Kuzaa ni suala la muda tu, kwa hiyo muda ukifika na Mungu akitaka nitazaa tu maana wakati wa Mungu ndiyo sahihi, mimi siyo tasa, nina watoto wawili kwa hiyo Mungu akijaalia nitamzalia mume wangu Uchebe tu,” alisema Shilole.

Stori: Mwandishi Wetu
Toa comment