Shoo Ya Jide ilivyofunika Mlimani City Alfajili Ya Leo

2 0Shoo Ya Jide ilivyofunika Mlimani City Alfajili Ya Leo

Maunda Zorro ndiye aliyeanza kukamua kabla ya Jide.

Mkongwe wa Bongo Fleva, Lady Jaydeee Komando, usiku wa kumkia leo alipiga bonge la shoo kwenye Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar akisherehekea kutimiza miaka 20 kwenye gemu.

Jide alipovamia jukwaa.

Shoo hiyo ilihudhuriwa na nyomi la mashabiki ambapo mwanamuziki huyo aliwanogesha ile mbaya.

Mashabiki wakifurahia shoo.

Shoo hiyo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali wa Bongo muvi, Bongo Fleva na wengine ambapo Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Geofrey Mungereza a.k.a Mzee wa Rungu la Maadili naye alikuwepo akiifutilia kiumakini shoo hiyo.

Katibu Mtendaji wa Basata Geofrey Mungereza akifurahia shoo hiyo.

Baadhi ya mastaa walihudhuria ni wasanii wa Bongo muvi, Kajala Masanja, Steve Nyerere, Mwanamitindo Flaviana Matata na wengine wengi.

Zuchu naye alipanda jukwaani kunogesha shoo hiyo.

Jide akikamua na AY.

Msanii Kajala Masanja (kushoto) na Shostito wake hivi ndivyo walivyonaswa.

Pedeshee Daud Mambya (kushoto) naye akiwa kwenye pozi na Shostito kwenye shoo hiyo.

HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL   Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *