Shoo ya Mzee Yusuf Yasogezwa Mbele Dar Live

LEO shoo babkubwa iliyokuwa ifanyike Julai 7 mwaka huu, imesogezwa mbele kutokana na kuomboleza kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa aliyefariki usiku wa kuamkia Ijumaa.

 

Akizungumza na Championi Jumatano,mratibu wa shoo hiyo, Rajab Mteta ’KP’ alisema wameamua kusitisha shoo hiyo kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao, ambapo wao kama uongozi wanaungana na taifa kwa ujumla kuomboleza kifo cha hayati Mkapa.

“ Shoo ilitakiwa iwe Julai 7 mwaka huu, kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wetu shoo imesogezwa mbele na itafanyika siku ya mkesha wa nanenane, tunaomba mashabiki wa mzee Yusuf wafi ke kwa wingi Viwanja vya Dar Live Mbagala-Zakhiem siku hiyo mfalme wa muziki wa Taarabu atapata nafasi ya kutambulisha nyimbo zake mpya,” alisema.

 

Mzee Yusuf alisema: “ Naomba mashabiki zangu wafi ke kwa wingi, kama mnavyojua huwa sina kazi mbovu mjini, mfalme narudi tena narudi kwa kishindo kikubwa, ” alisema.

Stori: Memorise Richard, Dar es SalaamToa comment