Shoo ya Nandy Yaiteka Arusha NCBA ikizindua Matawi Mapya

6 0Shoo ya Nandy Yaiteka Arusha NCBA ikizindua Matawi Mapya

Msanii wa kizazi kipya Faustina Charles Mfinanga maarufu Nandy mwishoni mwa wiki iliyopita alipiga bonge la shoo kwenye hafla ya uzinduzi wa matawi mawili mapya ya Benki ya NCBA Tanzania Limited.

Benki hiyo ilifanya uzinduzi huo jijini Arusha jumamosi ya Septemba 19 mwaka huu.

Matawi haya mawili mapya ni Tawi la Clock Tower lililopo Fire Road, Jengo la TFA na Tawi la Sokoine lililopo barabara ya Sokoine, Central Plaza ghorofa ya chini.

Hafla hiyo ya uzinduzi huo ni miongoni mwa matukio yanayoendelea kusherekea ujio wa Benki ya NCBA, ambayo ni muunganiko wa hiari kati ya NIC (T) Limited na CBA Bank (T) Limited ambapo huduma rasmi za taasisi hii mpya ya Kifedha zilianza Julai 8, 2020 baada ya idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Wageni waalikwa wakifurahia shoo ya Nandy.

Mgeni rasmi wa hafla hiyo alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Dkt Hamisi Kigwangalla ambaye aliisifu Benki ya NCBA kwa juhudi zao za kuchochea uchumi wa Tanzania.

Alisema, ‘Benki ya NCBA imewasili nchini kwa wakati sahihi kabisa mara tu baada ya Tanzania kujumuishwa kama nchi yenye kipato cha kati huku kukiwa na kiu cha kichocheo kipya kitakachoimarisha nafasi yetu mpya  kiuchumi’.

Waziri alielezea kwa kina sehemu muhimu zinazohitaji msaada wa kifedha mkoani Arusha baada ya athari za ugonjwa wa COVID-19. Alisema Kigwangalla.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha, Mhe Richard Kwitega aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe Idd Hassan Kimanta aliyekuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika hafla hiyo.

Waziri Kigwangalla na Margret Karume (katikati) wakati wa uzinduzi huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja wa benki hiyo na kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kitwega.

Katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Benki ya NCBA Bi Margaret Karume, aliwashukuru sana wenyeji wa mkoa huo na wageni waheshimiwa kwa kuhudhuria hafla hiyo.

Benki ya NCBA imezindua matawi 2 mkoani Arusha, yakiwa miongoni mwa matawi 12 mapya nchini baada ya kuzindua Makao ya Makuu ya ofisi na tawi mkoani Dar es Salaam mnamo Agosti 19 mwaka huu. Benki ya NCBA inatazamia katika siku zijazo kuzindua matawi yake mapya ambayo tayari yameanza kutoa huduma katika mkoa wa Mwanza na visiwani Zanzibar.Toa comment

Posted from

Related Post

Ed Sheeran Atangaza Kupumzika Muziki

Posted by - August 29, 2019 0
Ed Sheeran Atangaza Kupumzika Muziki August 29, 2019 by Global Publishers MWANAMUZIKI maarufu duniani, Mwingereza, Edward Christopher Sheeran,  maarufu kama…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *