Shughuli ya H-Baba Uzinduzi Kampeni za Shigongo Buchosa – Video

MSANII wa Bongo Fleva, H Baba, amekiwasha kwenye uwanja wa Nyakaliro wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge wa Jimbo la Buchosa (CCM),  Eric Shigongo, leo Ijumaa, Septemba 25, 2020.

 

Wananchi wa Buchosa wamefurika katika viwanja hivyo kusikiliza kampeni za mgombea wao ili wafanye maamuzi sahihi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.

 

Katika uzinduzi huo, Shigongo ameambatana na mkewe, Veneranda Ephraim, viongozi waandamizi wa CCM Wilaya ya Sengerema na Buchosa, mgombea ubunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku ‘Msukuma’ na aliyewahi kuwa mbunge wa Nyamagana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Marsha.

 
Toa comment