Silva, Jesus na Garcia kumng’oa Messi Barcelona

1 0

Inadaiwa Manchester City imeandaa ofa ya paundi milioni 89.5, ikiwa sanjari na wachezaji watatu Bernardo Silva, Gabriel Jesus na Eric Garcia kwenda Barcelona ili tu kumsajili mshambuliaji wao hatari na ambaye ametangaza kutaka kuondoka Lionel Messi.

City inamatumaini ya kufikia makubaliano na miamba hii ya Catalan baada ya Messi mwenyewe kutangaza kutaka kuondoka ndani ya klabu hiyo msimu huu.

Endapo Messi atakubaliana na City, atakwenda kuungana na kocha wake wa zamani Pep Guardiola ambaye kupitia yeye alikuwa na mafanikio makubwa kwenye tasnia yake ya kusakata soka ndani ya Nou Camp akifunga jumla ya magoli 634, na assists 285 katika mechi 731 alizocheza.

Man City 'are ready to offer £89.5m PLUS B Silva, Jesus and Garcia for Messi| All Football

Bongofive inafahamu kuwa wawili hao wanadaiwa kuwa na mawasiliano kupitia njia ya simu kuhusu kujiunga na Etihad, hata pia mazungumzo ya jinsi gani Messi ataweza kuishi England na kujifunza lugha ya Kiingereza baada ya kuishi Hispania kwa miaka 20.

Wazo la City kumsaini Messi linaonekana kuwa ilikuwa ndoto za muda mrefu, lakini kwa dau hili la paundi milioni 89.5 likiwa pamoja na wachezaji Silva, Jesus na Garcia linaweza kutimiza malengo yao ya usajili.

Kwa mujibu wa Sport, mawasiliano yamefanywa na kiongozi wa Barca kumleta Jesus ndani ya Nou Camp. Jesus amekuwa ni tageti namba moja kwa wa Catalans hao ili kuchukua nafasi ya Luis Suarez.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *