SIMBA: HAIKUWA BAHATI YETU LEO YATOKA SARE NA US DO SONGO

KOCHA wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa haikuwa bahati yao kushinda leo kutokana na kubwanwa na wapinzani wao kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa nchini Msumbiji.

 

Simba leo walikaribishwa na US do Songo ya Msumbiji kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika uiochezwa uwanja wa Beira.

 

Akizungumza mara baada ya mchezo wa leo, uliochezwa uwanja wa Beira, Aussems amesema kuwa jitihada za wachezaji zimegonga mwamba kwao kupata matokeo.

 

“Kwa kiasi chake wachezaji wamepambana licha ya kukosa ushindi, kuna mambo madogo ambayo hayajafanyiwa kazi hivyo tunajipanga kwenye mchezo wa marudio,” amesema.

 

Simba imelazimisha sare tasa ya bila kufungana baada ya ubao kusoma kwa Ud Songo 0 sawa na Simba, mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25 uwanja wa Taifa.

Toa comment