SIMBA OUT LIGI YA MABINGWA, YATOKA 1-1 UD SONGO TAIFA

25 0

SIMBA OUT LIGI YA MABINGWA, YATOKA 1-1 UD SONGO TAIFA

RASMI leo Simba imetolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye mchezo wa marudio uliochezwa uwanja wa Taifa.

Simba inatolewa na UD Songo kwa faida ya bao la ugenini ambalo wamelipata leo huku Simba wakiwa hawaamini wanachokiona.

 

Leo Simba walitakiwa kupata ushindi wa aina yoyote na kulinda bao lao mwisho wa siku walikubali kufungwa dakika ya 14 kwa uzembe wa mabeki ambao waliusindkiza kwa macho mpira wa adhabu uliopigwa na nahodha wa UD Songo, Luis dakika ya 14.

Bao lao la usiku lilifungwa na Erasto Nyoni dakika ya 87 halikusaidia kuivusha hatua ya leo kutokana na kutokuwa na bao la faida walilopata kwenye mchezo wa kwanza.

 

Sasa Simba itaungana na KMC ambayo nayo ilitolewa uwanja wa Taifa kwa kufungwa mabao 2-1 na AS Kigali kuzipa sapoti timu mbili za Tanzania zilizosonga hatua ya mbele ambazo ni Yanga pamoja na Azam FC.

 

Patrick Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa haikuwa bahati yao leo kushinda kwani wamepoteza nafasi nyingi za wazi.

Loading…

Toa comment

Posted from

Related Post

Dorah Atamani Mtoto wa Kike

Posted by - February 8, 2020 0
Dorah Atamani Mtoto wa Kike February 8, 2020 by Global Publishers MWANADADA mwenye umbo dogo kutoka Bongo Movie, Wanswekula Zacharia…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *