Simba Yamzuia Beki Kucheza Yanga

IMEFICHUKA rasmi kuwa uongozi wa Yanga uliamua kumuweka benchi beki wao wa kushoto, rasta Yassin Mustapha katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union ili asiukose mchezo uliokuwa unafuata wa ligi dhidi ya Simba kutokana na kuwa na kadi mbili za njano.

 

Yassin katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Kagera na Mtibwa Sugar alipata kadi mbili za njano, jambo ambalo lilikuwa linahatarisha kuukosa mchezo unaofuata dhidi ya Simba kama angefanikiwa kuipata kadi ya tatu ya njano dhidi ya Coastal Union lakini hata hivyo mechi hiyo imesogezwa hadi Novemba 7, mwaka huu.

 

Yanga katika mchezo huo ilimtumia beki mwingine wa kushoto Adeyun Saleh, ambapo walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo aliyekuwa kocha wa timu hiyo Zlatko Krimpotic, alisema kuwa walihofi a kumtumia mchezaji huyo ili wawe na uhakika wa kumtumia katika mchezo unaofuata.

 

“Tusingeweza kumtumia Yassin Mustapha, kisha acheze kwa tahadhari akiwa anawaza tahadhari ya kupata kadi, nahisi hata yeye asingeweza kucheza vizuri kama angepewa nafasi ya kucheza katika mchezo dhidi ya Coastal.

 

“Tulichofanya sisi ni kuhakikisha kuwa tunamuweka nje ili kuwe na uhakika wa kumtumia katika mchezo unaofuata dhidi ya Simba, tunashukuru nafasi yake amecheza Adeyun ambaye pia ni mchezaji mzuri katika nafasi yake,” alisema kocha huyo ambaye baadaye alitimuliwa.

MARCO MZUMBE, Dar es SalaamTecno


Toa comment