Skendo Nzito Gari la Dada wa Mondi

8 0Skendo Nzito Gari la Dada wa Mondi

Dar: Jambo limezua jambo! Lile gari la kifahari aina ya BMW X5 ambalo alizawadiwa dada wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Khan pamoja na mumewe kwenye sherehe ya harusi yao, limeibuliwa skendo nzito, Gazeti la IJUMAA limedaka mchapo kama wote!

 

Esma ambaye ni mjasiriamali mwenye umaarufu wake mjini, alizawadiwa gari hilo kwenye sherehe iliyofanyika Agosti 5, mwaka huu katika Ukumbi wa Golf, Lugalo jijini Dar.

 

VYANZO VYAIBUA SKENDO

Vyanzo mbalimbali ambavyo vilizungumza na Gazeti la IJUMAA, vilishusha madai mazito kuwa, gari hilo lilikuwa bosheni na lilitolewa tu kama maonesho siku ya sherehe kuwahadaa wageni waalikwa waone kwamba, pesa ipo.

 

“Ni chezo, lile lilichezwa bwana. Hakukuwa na gari pale. Lile walileta tu pale kama kuchangamsha sherehe tu, baada ya hapo gari likarudishwa yadi,” chanzo kimoja kililitonya IJUMAA.

 

DATA ZATOLEWA…

Chanzo kingine kilienda mbele zaidi kwa kutoa data ambazo zinasherehesha hoja ya msingi kwamba, gari lilikuwa bosheni, kwani hakuna mahali popote ambapo Esma ameliposti toka siku ile.

“Wewe fuatilia, Esma kwenye ukurasa wake wa Instagram umeshaona ameliposti lile gari au hata kuonekana nalo mitaani? Ushamuona nalo hata pale dukani kwake Afrika Sana? Bosheni lile niamini mimi,” kiliweka nukta chanzo hicho.

 

IJUMAA MZIGONI

Baada ya kupata madai hayo mazito ambayo yanaigusa moja kwa moja familia ya Diamond au Mondi ambayo inaaminika wapo vizuri kiuchumi, IJUMAA lilianza kuifanyia kazi habari hiyo katika maeneo tofauti.

 

Kwanza; IJUMAA lilijiridhisha kwa kuperuzi kwenye ukurasa wa mrembo huyo na kubaini kweli hajawahi kuliposti gari hilo licha ya kuwa mastaa wengi wamekuwa na kawaida ya kuposti matukio mbalimbali wanapokuwa matembezini.

 

Pili; kwenye misele yake ambayo Esma ameonekana kuipiga hivi karibuni licha ya kudaiwa kwamba, hajafika kwenye biashara yake ya duka lililopo maeneo ya Sinza Afrika Sana, ilielezwa kuwa, haonekani na hilo gari jipya.

 

MWENYEWE ANASEMAJE?

Baada ya kuona madai yanazidi kuwa mengi, IJUMAA lilimtafuta Esma mwenyewe, ambapo alipoulizwa kuhusiana na gari hilo, alishusha povu kama lote akihoji kama kuna mtu yeyote alishawahi kumuona tangu afunge ndoa.

 

“Hivi watu ambao wanashadadia sana kuhusiana na mambo yangu, walishawahi kuniona hata kidogo kwenye mitandao au hata mitaani tangu niolewe?

Sasa wanazungumziaje kuhusu gari nililopewa hawalioni?” alihoji Esma.

 

ABADILIKA KIDOGO…

Akiendelea kuzungumza, Esma alisema kuwa, hata hivyo ameagiza gari nyingine kutoka nchini Afrika Kusini kwa sababu lile alilozawadiwa siku ya harusi (BMW X5) hakulipenda, hivyo ameagiza la gharama ya juu zaidi.

 

“Ukweli ni kwamba, gari ambalo nilipewa sikulipenda, hivyo nikaamua kuagiza lingine ambalo ni la kufunuka juu, na lina gharama kushinda lile na hivi karibuni litafika, watu wataliona,” alisema Esma ambaye alisisitiza bado anakula fungate.

 

TUJIKUMBUSHE

Siku ya sherehe, ilipofika wakati wa kutoa zawadi, alitokea jamaa mmoja upande wa mwanaume ambaye alijitambulisha kwa jina la Bobo, akaanza kujinasibu kuwa wamemzawadia Esma na mumewe gari hilo.

Lakini wakati akijitapa kutoa gari hilo, Mondi aliingilia kati kwa kuchukua kipaza sauti na kusema kuwa, anashukuru mashemeji zake hao wamejitutumua lakini gari hilo ni la kawaida.

 

Mondi alisema gari hilo yeye aliwahi kupewa mwaka 2014, na kuonesha kwamba, ameliona ni la kawaida, akasema anaongezea Dola 50, 000 ili ikiwezekana warudishe pesa zote walizonunulia gari hilo na chenchi ibaki.

Stori: IMELDA MTEMA, IjumaaToa comment

Posted from

Related Post

P Funk: Msishangae Siku Nikiokoka

Posted by - July 28, 2020 0
P Funk: Msishangae Siku Nikiokoka July 28, 2020 by Global Publishers PAUL Matthysse almaarufu kama P Funk, Halfani, Majani, Kinywele…

Niyonzima Avutiwa Na Rutanga Yanga

Posted by - June 23, 2020 0
Niyonzima Avutiwa Na Rutanga Yanga June 23, 2020 by Global Publishers Haruna Niyonzima. KIUNGO mchezeshaji fundi wa Yanga, Haruna Niyonzima,…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *