Snura: Mwanamke wa Kwanza Kuvalishwa Kofia na Rais – Video

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mgombea anayetetea kiti chake kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John  Magufuli leo Septemba 21, 2020 ameendelea na utaratibu wake wa kuwavalisha kofia wasanii katika kampeni zake.

 

Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, leo amewavalisha kofia zake wasanii Menja Kunta na Snura Mushi wakati wakitumbuiza katika kampeni hizo kwenye Uwanja wa Mirambo uliopo Urambo mkoani Tabora.

Baada ya tukio hilo Snura Mushi amejigamba na kuwa yeye amekuwa mwanamke wa kwanza kuvalishwa kofia na rais.

Kupitia ukurasa wake wa instagramu ameandika haya; ”Nashukuru sana kuwa mwanamke wa kwanza kuvishwa kofia na raisi wetu JPM… Msanii wa kwanza wa kike Rais kuvua kofia yake na kunivalisha, (hii ni kubwa sana kwangu).. Ndani ya mkoa wa TABORA sitosahau historia hii.

“Kwangu Mimi ni baraka kubwa sana nimepewa leo na Mh. Rais Dr John Pombe Magufuli kwa kuniheshimisha nashukuru sana tena sana, ama kwa hakika huyu ni Rais mwenye upendo sana, na kupitia chama changu cha MAPINDUZI leo nimepata heshima hii kubwa kama mwanamke…

 

Asanteni sana viongozi wangu wote wa chama🙏🙏.. “Hakika Mungu akitaka kukuheshimisha hakuna anaeweza kukudharaulisha alhamdulillah Mungu umenijibu jibu kubwa sana. CCM OYEEE 💚💚 MAGUFULI OYEEE..” @snuramushiToa comment