Sonia ni Staa Tangu Azaliwe!

MWIGIZAJI mkongwe wa Bongo Movies, Yvonne Cherry ‘Monalisa’, amefunguka kuwa, mwanaye Sonia alikuwa staa tangu anazaliwa.

 

Akipiga stori na OVER ZE WEEKEND, Monalisa au Mona amesema umaarufu wa Sonia unaweza ukawa hujaanza kipindi hiki alichoanza kuimba Bongo Fleva, bali ni wa tangu anazaliwa.

 

“Unajua Sonia amekuwa maarufu tangu anazaliwa; yaani alikuwa anatoka sana kwenye magazeti, kipindi hicho ndoa yangu na marehemu George Tyson ambaye ni baba yake, ilikuwa iko hot sana, naweza kusema hiyo ndiyo sababu ya yeye kupata umaarufu pia,’’ anasema Mona.

STORI: HAPPYNESS MASUNGAToa comment