Stamina: Naweza Kusimama Bila Roma

RAPA mkali Bongo, Bonventure Kabogo ‘Stamina Shorwe-bwenzi’ amejimwambafai kuwa, anaweza kusi-mama mwenyewe bila rapa mwenzake, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ wanaounda muunganiko wa ROSTAM.

 

Akistorisha na OVER ZE WEEKEND, Stamina amesema, kuna watu wana mtazamo huo kuwa hawezi kusimama kwenye muziki wake bila Roma ambaye kwa sasa maskani yake yapo nchini Marekani.

 

“Nimeanza kufanya muziki muda mrefu bila kuwa kwenye kundi. Sasa kwa nini watu waseme kuwa siwezi kusonga mbele kwa sababu mwenzangu ameenda kuishi nchi nyingine? Tayari kuna ngoma ambazo zinafanya poa na nimesimama mwenyewe,” anasema Stamina ambaye ametisha kwenye ngoma yake ya Asiwaze.

STORI: HAPPYNESS MASUNGA
Toa comment