Sven Aweka Hesabu Kali Dakika 540 Bongo

KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, amebainisha kuwa licha ya kwamba wamepata sare kwenye mechi yao na Mtibwa Sugar, hesabu zake ni ndani ya mechi sita, sawa na dakika 540, wawe tayari wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara.

 

Kocha huyo ameongeza kwamba hayo ndiyo malengo yake na anajua wazi atayafikia licha ya kupata sare na Mtibwa Sugar.

 

Simba kwa sasa ina pointi nne baada ya kushinda mechi moja na Ihefu na sare moja dhidi ya Mtibwa Sugar. Kocha huyo raia wa Ubelgiji amesema kuwa plani zake kwa wakati huu ni ndani ya mechi zao hizo sita wawe tayari wanaongoza ligi na kujiweka eneo la kutetea ubingwa wao.

 

“Plani tulizonazo ni kuwa baada ya mechi kuanzia tano au sita tunataka kuona tunaongoza Ligi. “Tunajua haitakuwa rahisi lakini tutapambana kulifanikisha hilo, bila ya kujali aina ya matokeo ambayo tutayapata,” alimaliza Sven. Mechi sita zijazo za Simba ni dhidi ya Biashara United, Gwambina, JKT Tanzania, Prisons, Yanga na Ruvu Shooting.

SAID ALLY, Dar es SalaamToa comment